ALIKUWA MPENZI WAKO, KWA NINI SASA UMHARIBIE?

WAPENZI wa XXXLove tunakutana tena leo kwa rehema na kudra za Maulana. Nami bila hiyana nawakaribisha wasomaji wangu kwa moyo mkunjufu, karibuni!

Leo nitazungumza na watu ambao walikuwa na mahusiano mwanzoni, baadaye mapenzi yao yakafika mwisho na
kila mtu kuanza maisha yake mapya.

Kwa bahati nzuri mwenza wako kaolewa ama kuoa na wewe bado uko bachela, kwa nini uanze kumsumbua? Hilo ni tatizo, tena tatizo kubwa sana ambalo kama hautalitambua unaweza kujiingiza pabaya.

Niseme tu kwamba, yeyote wenye tabia hiyo, ni mjinga na mshamba wa hali ya juu. Kama mwenzi wako ameshaolewa au kuoa muache afurahie maisha ya ndoa na familia yake, ya nini kumsumbua kujifanya unampenda wakati mliachana?

Usijifanye kumpenda sana wakati hata akitoka kwa mumewe huwezi kumuoa. Kama ulimpenda kwa dhati si ungemuoa ama kuolewa naye? Kama ulihitaji awe wako si ungemvumilia kwa shida na raha badala ya kumkimbia?

Alikosa nini ukamuacha na sasa amebadilika nini unamsumbua? Kumbuka ulimuona wa nini wenzio wamemuona wa thamani, kisebusebu cha nini tena?

Leo kapata mpenzi mwingine anayempenda kwa dhati, unaanza kumsumbua ili hali ukijua mwenzio kaolewa ama kaoa.

Mimi nadhani ifike sehemu uwe na heshima, kama kaolewa ama kuoa si busara kuingilia uhusiano wake. Tambua yawezekana mlijiingiza katika uhusiano kwa sababu ya umri na tamaa zenu za ujanani, lakini ukweli hamkuwa na malengo yoyote ya baadaye na ndiyo maana hamkufikia maisha ya ndoa.

Kila jambo na wakati wake, kujifanya unamjua zaidi mke au mume wa mtu wakati ana ndoa yake ni kujitafutia matatizo.

Kwanza ni ujinga na ushamba, pili ulimbukeni wa kuparamia vya watu ambao unaweza kukufanya yakakukuta makubwa na ukajutia.

Kama alikuwa wako basi ni zamani, kama alikuwa mpenzi wako basi ni utotoni, shuleni, chuoni, madrasa au kwenye kwaya, kwa sasa ana ubavu wake hivyo kuwa na heshima.

Hivi unawezaje kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenye simu ya mke au mume wa mwenzio, tena muda mbaya wakati X-wako kwa sasa ana familia yake?

Je, furaha yako ni kuvuruga ndoa yake au ni nini hasa ulicholenga katika familia yake?

Natamani wewe unayefanya hivyo uoe au uolewe kisha aliyekuwa mpenzi wa huyo uliyeingia naye kwenye ndoa aanze kumtumia sms za kimapenzi halafu tuone kama utafurahia.

Ukweli ulio wazi ni kwamba, utaumia sana na unaweza kuamua hata kumuacha huyo mwenza wako.

Sasa basi kama wewe utaumia, kwa nini umfanyie mwenzako hivyo? Acha ushamba! Kama alikuwa wako ni enzi hizo, sasa hivi ana mtu wake na anayafurahia maisha, usimsumbue.

Naamini ujumbe wangu umefika na kila mwenye tabia hiyo ataacha mara moja.

WAPENZI wa XXXLove tunakutana tena leo kwa rehema na kudra za Maulana. Nami bila hiyana nawakaribisha wasomaji wangu kwa moyo mkunjufu, karibuni!

Leo nitazungumza na watu ambao walikuwa na mahusiano mwanzoni, baadaye mapenzi yao yakafika mwisho na kila mtu kuanza maisha yake mapya.

Kwa bahati nzuri mwenza wako kaolewa ama kuoa na wewe bado uko bachela, kwa nini uanze kumsumbua? Hilo ni tatizo, tena tatizo kubwa sana ambalo kama hautalitambua unaweza kujiingiza pabaya.

Niseme tu kwamba, yeyote wenye tabia hiyo, ni mjinga na mshamba wa hali ya juu. Kama mwenzi wako ameshaolewa au kuoa muache afurahie maisha ya ndoa na familia yake, ya nini kumsumbua kujifanya unampenda wakati mliachana?

Usijifanye kumpenda sana wakati hata akitoka kwa mumewe huwezi kumuoa. Kama ulimpenda kwa dhati si ungemuoa ama kuolewa naye? Kama ulihitaji awe wako si ungemvumilia kwa shida na raha badala ya kumkimbia?

Alikosa nini ukamuacha na sasa amebadilika nini unamsumbua? Kumbuka ulimuona wa nini wenzio wamemuona wa thamani, kisebusebu cha nini tena?

Leo kapata mpenzi mwingine anayempenda kwa dhati, unaanza kumsumbua ili hali ukijua mwenzio kaolewa ama kaoa.

Mimi nadhani ifike sehemu uwe na heshima, kama kaolewa ama kuoa si busara kuingilia uhusiano wake. Tambua yawezekana mlijiingiza katika uhusiano kwa sababu ya umri na tamaa zenu za ujanani, lakini ukweli hamkuwa na malengo yoyote ya baadaye na ndiyo maana hamkufikia maisha ya ndoa.

Kila jambo na wakati wake, kujifanya unamjua zaidi mke au mume wa mtu wakati ana ndoa yake ni kujitafutia matatizo.

Kwanza ni ujinga na ushamba, pili ulimbukeni wa kuparamia vya watu ambao unaweza kukufanya yakakukuta makubwa na ukajutia.

Kama alikuwa wako basi ni zamani, kama alikuwa mpenzi wako basi ni utotoni, shuleni, chuoni, madrasa au kwenye kwaya, kwa sasa ana ubavu wake hivyo kuwa na heshima.

Hivi unawezaje kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenye simu ya mke au mume wa mwenzio, tena muda mbaya wakati X-wako kwa sasa ana familia yake?

Je, furaha yako ni kuvuruga ndoa yake au ni nini hasa ulicholenga katika familia yake?

Natamani wewe unayefanya hivyo uoe au uolewe kisha aliyekuwa mpenzi wa huyo uliyeingia naye kwenye ndoa aanze kumtumia sms za kimapenzi halafu tuone kama utafurahia.

Ukweli ulio wazi ni kwamba, utaumia sana na unaweza kuamua hata kumuacha huyo mwenza wako.

Sasa basi kama wewe utaumia, kwa nini umfanyie mwenzako hivyo? Acha ushamba! Kama alikuwa wako ni enzi hizo, sasa hivi ana mtu wake na anayafurahia maisha, usimsumbue.

Naamini ujumbe wangu umefika na kila mwenye tabia hiyo ataacha mara moja.

GPL
Share:

No comments:

Post a Comment

BLOG VIEWERS

RECENT POSTS

Popular Posts

BLOG RAFIKI