Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, Bw. George Nyatega
Na Mwandishi Wetu
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa, Mei 1,
2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo
na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa
masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.
masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz),
waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao
kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.
Aidha,
wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na
kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online
Loans Application and Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili
ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au
kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).
Pamoja
na mambo mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya
kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs
30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia
katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.
“Waombaji
wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo
inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema
sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.
Aidha,
mwongozo huo umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na
masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha
maombi tena.
Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.
HESLB
ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi
mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa
wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha,
jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa
wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali
ilipoanza kukopesha wanafunzi.
No comments:
Post a Comment